Swali: Ni ipi hukumu ya Kiislamu kwa anayejenga nyumba katika makaburi?

Jibu: Makaburi hayajengwi ndani yake. Bali inapaswa kuondoa majengo yoyote yaliyopo humo. Ni jukumu la serikali, viongozi wa manispaa, taasisi za hisba na viongozi wa maeneo kuhakikisha jambo hili. Makaburi yanapaswa kuheshimiwa, kulindwa na kuwekwa uzio. Hayajengwi ndani yake nyumba, maduka au chochote kingine. Yabaki kwa wenye makaburi, kwani huo ndio makazi yao na sehemu yao.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1142/حكم-بناء-البيوت-في-المقابر
  • Imechapishwa: 03/01/2026