Swali: Je inajuzu kusema “Ndio” katika Suurah zinazoishia kwa maswali, kama Aayah:
أَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَحْكَمِ الْحَاكِمِينَ
”Je, kwani Allaah si Mwadilifu zaidi kuliko mahakimu wote?”[1]
na kama ilivyo kusema “Aamiyn” baada ya kusoma al-Faatihah?
Jibu: Ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah isipokuwa wakati wa kusoma Aayah ya mwisho katika Suurah al-Qiyaamah, nayo ni maneno Yake (Ta´ala):
أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ
“Je, huyo hakuwa ni muweza wa kuhuisha wafu?”[2]
Inapendekezwa wakati wa kuisoma kusema:
سبحانك فبلى
“Kutakasika ni Kwako, ndio.”[3]
Kwa sababu Hadiyth imesihi juu ya hilo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] 95:08
[2] 75:40
[3] Ahmad (7342) na Abu Daawuud (887).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/286)
- Imechapishwa: 08/03/2026
Swali: Je inajuzu kusema “Ndio” katika Suurah zinazoishia kwa maswali, kama Aayah:
أَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَحْكَمِ الْحَاكِمِينَ
”Je, kwani Allaah si Mwadilifu zaidi kuliko mahakimu wote?”[1]
na kama ilivyo kusema “Aamiyn” baada ya kusoma al-Faatihah?
Jibu: Ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah isipokuwa wakati wa kusoma Aayah ya mwisho katika Suurah al-Qiyaamah, nayo ni maneno Yake (Ta´ala):
أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ
“Je, huyo hakuwa ni muweza wa kuhuisha wafu?”[2]
Inapendekezwa wakati wa kuisoma kusema:
سبحانك فبلى
“Kutakasika ni Kwako, ndio.”[3]
Kwa sababu Hadiyth imesihi juu ya hilo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] 95:08
[2] 75:40
[3] Ahmad (7342) na Abu Daawuud (887).
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/286)
Imechapishwa: 08/03/2026
https://firqatunnajia.com/kuitikia-ndio-katika-aayah-ya-mwisho-ya-suurah-al-qiyaamah-na-at-tiyn/