Swali: Ni yepi malipo kwa mwenye kuchoma moto Qur-aan tukufu kwa kusahau na wala hakujua kitendo hicho isipokuwa baada ya kukifanya?
Jibu: Hakuna kinachomlazimu muda wa kuwa ameichoma kwa kusahau au ameichoma kwa kukusudia kwa sababu imechanikachanika na hanufaiki kwayo na hivyo akaichoma kwa sababu isitwezwe. Katika hali hiyo hakuna neno. Kwa sababu Qur-aan imekatikakatika na imechanikachanika na hanufaiki kwayo, inatiwa moto. Pia mtu anaweza kuifukia kwenye ardhi safi ili isitwezwe. Ikiwa aliichoma kwa kusahau hakujua kuwa ni Qur-aan hakuna dhambi kwake.
Ama akiichoma moto kwa sababu ya kuitukana au kwa sababu ya kuichukia anaritadi kutoka nje ya Uislamu. Kama anaichoma kwa sababu ya kuichukia na kuibughudhi ni dhambi kubwa na ni kuritadi kutoka nje ya Uislamu. Vivyo hivyo endapo ataikalia, akaikanyaga kwa miguu kwa ajili ya kuidharau au akaitupa katika najisi, matendo yote haya ni kuritadi kutoka nje ya Uislamu.
Akipatikana muislamu ambaye anaidharau Qur-aan waziwazi kama kwa mfano kwa kuikanyaga kwa miguu yake, akaikalia kwa makalio yake, akaitupa katika najisi au akaitukana, akamtukana yule anayeizungumza au mfano wa hayo ni kuritadi kutoka nje ya Uislamu. Ni kufuru kubwa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: binbaz.org.sa/fatwas/7700/حكم-احراق-القران-سهوا-وعمدا
- Imechapishwa: 02/05/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Ibn ´Uthaymiyn aliyesahau Qur-aan baada ya kuhifadhi
Swali: Ni jambo linalojulikana kwamba wanafunzi wanakaririwa kitu kutoka katika Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall). Unapofika mwaka wa pili tunasahau baadhi ya Suurah tulizosoma mwaka uliopita klasini. Je, imeharamishwa kwa mtu kusahau baadhi ya Suurah hizi zilizokuwa zimethibiti? Jibu: Itambulike kuwa pindi Allaah anapomneemesha mtu kuhifadhi kitu kutoka katika…
In "Kisomo cha Qur-aan"
Amesoma al-Faatihah katika Tashahhud kwa kusahau
Swali: Kuna mtu amesoma al-Faatihah katika Tashahhud kwa kusahau. Je, arudi swalah yake? Jibu: Asiirudi swalah yake akisoma al-Faatihah katika Tashahhud kwa kusahau. Lakini hata hivyo ni wajibu kwake kusoma Tashahhud. Kwa sababu Tashahhud ya mwisho inayofuatiwa na salamu ni nguzo. Kuhusu Tashahhud ya kwanza au ya kati kati ni wajibu…
In "Tashahhud"
Kusahau Qur-aan aliyokuwa mtu amehifadhi
Swali: Mtu aliyehifadhi sehemu katika Qur-aan kisha akasahau anapata dhambi kwa hilo? Jibu: Hapati dhambi kwa hilo, lakini hii ni neema iliyomwondoka kwa sababu ya kuzembea. Ni juu yako kufanya bidii kuirudilia Qur-aan na kuihifadhi ili neema hii iweze kumrudilia.
In "Elimu na masomo"