Swali: Ni ipi hukumu ya kuhifadhi maeneo msikitini?
Jibu: Ikiwa mtu ambaye amehifadhi nafasi msikitini ametoka nje ya msikiti, kitendo hicho ni haramu kwake. Hakijuzu. Kwani hana haki ya nafasi hiyo. Nafasi inakuwa kwa yule ambaye ametangulia kuja mwanzo. Mpaka baadhi ya Hanaabilah wamefikia kusema kwamba ambaye anafanya hivo kisha akarudi na kuswali maeneo hayo, basi swalah yake ni batili. Kwa sababu amepora maeneo hayo. Hana haki ya maeneo hayo ilihali kuna mwingine ambaye kishamtangulia. Mtu anapaswa kuyatangulia maeneo kwa mwili wake, na si kwa mkeka wake, leso yake au bakora yake. Lakini kama mtu atakuwa msikitini na akaweka na akaweka vitu kama hivyo ilihali yuko ndani ya msikiti, lakini amefanya hivo ili aende mahali kwengine kwa ajili ya kusikiliza darsa au akote jua, basi kitendo hicho hakina neno kwa sharti asijipenyeze kati ya watu pindi ataporejea maeneo yake. Ikiwa itampelekea yeye kufanya hivo basi itamlazimu asubiri hadi pale ambapo itakuwa sawa safu ya mahali pake ili asiwaudhi watu.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/393)
- Imechapishwa: 12/04/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya kuhifadhi maeneo msikitini?
Jibu: Ikiwa mtu ambaye amehifadhi nafasi msikitini ametoka nje ya msikiti, kitendo hicho ni haramu kwake. Hakijuzu. Kwani hana haki ya nafasi hiyo. Nafasi inakuwa kwa yule ambaye ametangulia kuja mwanzo. Mpaka baadhi ya Hanaabilah wamefikia kusema kwamba ambaye anafanya hivo kisha akarudi na kuswali maeneo hayo, basi swalah yake ni batili. Kwa sababu amepora maeneo hayo. Hana haki ya maeneo hayo ilihali kuna mwingine ambaye kishamtangulia. Mtu anapaswa kuyatangulia maeneo kwa mwili wake, na si kwa mkeka wake, leso yake au bakora yake. Lakini kama mtu atakuwa msikitini na akaweka na akaweka vitu kama hivyo ilihali yuko ndani ya msikiti, lakini amefanya hivo ili aende mahali kwengine kwa ajili ya kusikiliza darsa au akote jua, basi kitendo hicho hakina neno kwa sharti asijipenyeze kati ya watu pindi ataporejea maeneo yake. Ikiwa itampelekea yeye kufanya hivo basi itamlazimu asubiri hadi pale ambapo itakuwa sawa safu ya mahali pake ili asiwaudhi watu.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/393)
Imechapishwa: 12/04/2026
https://firqatunnajia.com/kuhifadhi-maeneo-msikitini/