Swali: Mtu akinuia kutawadha na kuoga na wakati wa kuoga akagusa dhakari yake. Je, nia ya wudhuu´ wake inaharibika na hivyo ni wajibu kwake kutawadha tena baada ya kumaliza kuoga au kugusa dhakari hakuathiri wudhuu´ isipokuwa ikiwa kama mtu atafanya hivo baada ya wudhuu´ na si katikati yake?
Jibu: Mtu akinuia kuoga kisha akatawadha wudhuu´ wa swalah, halafu baada ya hapo akaoga na kugusa tupu yake kwa mkono wake moja kwa moja au akatokwa na manii, basi atatakiwa kutawadha tena. Haya ndio maoni ya sawa. Ama akishatawadha na asitokwe na upepo na wala asiguse tupu yake kwa mkono wake moja kwa moja hakuna neno.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (06) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/433/433.mp3
- Imechapishwa: 07/12/2018
Swali: Mtu akinuia kutawadha na kuoga na wakati wa kuoga akagusa dhakari yake. Je, nia ya wudhuu´ wake inaharibika na hivyo ni wajibu kwake kutawadha tena baada ya kumaliza kuoga au kugusa dhakari hakuathiri wudhuu´ isipokuwa ikiwa kama mtu atafanya hivo baada ya wudhuu´ na si katikati yake?
Jibu: Mtu akinuia kuoga kisha akatawadha wudhuu´ wa swalah, halafu baada ya hapo akaoga na kugusa tupu yake kwa mkono wake moja kwa moja au akatokwa na manii, basi atatakiwa kutawadha tena. Haya ndio maoni ya sawa. Ama akishatawadha na asitokwe na upepo na wala asiguse tupu yake kwa mkono wake moja kwa moja hakuna neno.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (06) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/433/433.mp3
Imechapishwa: 07/12/2018
https://firqatunnajia.com/kugusa-tupu-baada-ya-kumaliza-kuoga-josho-kubwa-na-kutawadha/