Imamu kuchunga hali watu wazima katika swalah ya kupatwa kwa jua

Swali: Sisi ni wanaume watuwazima na imamu anarefusha swalah ya kupatwa kwa jua. Je, imependekezwa achunge wale walio nyuma yake au ni lazima kurefusha?

Jibu: Ni lazima kurefusha ambako swalah ya kupatwa kwa jua itatofautiana na swalah nyingine. Ikiwa wengi walioko msikitini wako namna hii, yaani madhaifu na watuwazima, basi ichungwe hali yao. Ama ikiwa ni mmoja au wawili basi jambo hili ni sahali. Wakichoka kusimama wakae na waswali hali ya kukaa. Ama Sunnah kuachwa na swalah ya kupatwa kwa jua isipambanuke na swalah nyingine kwa njia ya kwamba ifupishwe mpaka iwe kama swalah zengine, hili ni jambo halitakikani. Ni lazima swalah ya kupatwa kwa jua iwe na sifa maalum zinazoipambanua na swalah zengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (49) http://binothaimeen.net/content/1112
  • Imechapishwa: 13/04/2019