Kufungua kwa aliyesafiri ndani ya Ramadhaan kwa ajili ya ´Umrah

Swali: Je, inajuzu kwa muislamu kwenda kufanya ´Umrah katika Ramadhaan, kisha afungue katika safari yake, au ni bora afunge na aache ´Umrah mpaka baada ya swawm?

Jibu: Kilicho bora ni kufanya ´Umrah katika Ramadhaan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”´Umrah ndani ya Ramadhaan ni sawa na Hajj.”

Imekuja katika riwaya nyingine:

”… ni sawa na kuhiji pamoja nami.”

Hii ni fadhilah kubwa sana.

Akisafiri, basi yuko huru kuchagua. Akipenda afungue njiani na akipenda afunge. Jambo hili lina upana. Akiwa Makkah hukumu ni hiyohiyo. Ikiwa atakaa Makkah kwa muda mfupi; siku mbili, tatu au nne, anaweza kufungua na anaweza kufunga. Ama ikiwa atakaa zaidi ya siku nne, basi atafunga akiwa Makkah na hafungui ikiwa amekusudia kukaa Makkah zaidi ya siku nne. Ama ikiwa anakusudia kufanya ´Umrah na kurejea, kukaa siku moja, siku mbili au tatu, basi ana ruhusa ya kufungua na ana ruhusa ya kufunga, yuko huru kuchagua.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1815/حكم-الافطار-لمن-سافر-في-رمضان-للعمرة
  • Imechapishwa: 23/02/2026