Swali: Je, kuna ubora kufunga Muharram yote? Je, nakuwa mzushi kwa kufanya hivo?
Jibu: Baadhi ya wanazuoni wanasema kuwa ni Sunnah kufunga Muharram yote. Wanajengea hoja kwa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Swawm bora baada ya Ramadhaan ni mwezi wa Allaah Muharram.”[1]
Hata hivyo kutokana na ninavojua ni kwamba haikupokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alifunga mwezi mzima. Mwezi unaofuata ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifunga sana ni mwezi wa Sha´baan, kama ilivyopokelewa katika Hadiyth Swahiyh kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa)[2]. Wala haitakiwi kumtuhumu ambaye amefunga mwezi mzima, kwa sababu Hadiyth iliyotajwa inaweza kueleweka kwa njia hiyo, kama walivosema baadhi ya wanazuoni, kufunga mwezi mzima.
[1] Muslim (1163).
[2] al-Bukhaariy (1969) na Muslim (1156).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/22)
- Imechapishwa: 19/03/2026
Swali: Je, kuna ubora kufunga Muharram yote? Je, nakuwa mzushi kwa kufanya hivo?
Jibu: Baadhi ya wanazuoni wanasema kuwa ni Sunnah kufunga Muharram yote. Wanajengea hoja kwa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Swawm bora baada ya Ramadhaan ni mwezi wa Allaah Muharram.”[1]
Hata hivyo kutokana na ninavojua ni kwamba haikupokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alifunga mwezi mzima. Mwezi unaofuata ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifunga sana ni mwezi wa Sha´baan, kama ilivyopokelewa katika Hadiyth Swahiyh kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa)[2]. Wala haitakiwi kumtuhumu ambaye amefunga mwezi mzima, kwa sababu Hadiyth iliyotajwa inaweza kueleweka kwa njia hiyo, kama walivosema baadhi ya wanazuoni, kufunga mwezi mzima.
[1] Muslim (1163).
[2] al-Bukhaariy (1969) na Muslim (1156).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/22)
Imechapishwa: 19/03/2026
https://firqatunnajia.com/kufunga-muharram-yote/