Swali: Mtu anayefuata kibubusa akimfuata mmoja wa wanazuoni katika suala fulani na wanazuoni wengine wanaona maoni mengine, kisha akamfuata yule wa kwanza kwa sababu ni nyepesi kwake. Je, tabia hii ni katika kufuata matamanio?

Jibu: Kufuata matamanio hakujuzu. Ni lazima kwake ajitahidi kumfuata yule anayemcha Allaah zaidi na mwenye uelewa zaidi akiwa hana uwezo.

Swali: Mfano baadhi ya makundi hubainikiwa na njia ya Sunnah na njia ya mfumo, hata hivyo wakashikilia kufuata kundi?

Jibu: Yule anayefuata matamanio anayo sehemu katika matashio ya Allaah. Ni lazima amche Allaah na afuate kile anachoona kuwa karibu zaidi na haki. Ikiwa ni mtu wa kawaida, basi aangalie wanazuoni na yule ambaye anaona moyoni mwake kuwa karibu zaidi na kheri na ni mwenye kumcha Allaah zaidi, ndiye amfuate.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31058/هل-من-اتباع-الهوى-الاخذ-بالايسر-من-الفتاوى
  • Imechapishwa: 27/09/2025