Kufanya kazi mwendo wa kilomita 100 na kujumuisha swalah

Swali: Kuna mtu anasafiri kila siku kilomita 100 kwenda kazini mwake. Anarudi nyumbani kabla ya swalah ya ´Aswr. Je, inajuzu kwake kujumuisha Dhuhr na ´Aswr?

Jibu: Maadamu ni msafiri inajuzu kwake kujumuisha Dhuhr na ´Aswr. Ni sawa pia kuswali Dhuhr njiani na ´Aswr nyumbani. Ana khiyri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir-ayat-10-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/06/2020