Swali: Mwanamke anaumwa kisukari na shinikizo la damu na ni mjamzito wa miezi saba. Madaktari wamemwambia kwamba mtoto wake hana fuvu na atakufa mara tu atakapozaliwa. Je, inajuzu kuavya?
Jibu: Mambo haya hayatakikani kuyachukulia wepesi. Madaktari wengi husema mambo yasiyo ya kweli; inahusiana na dhuluma na tuhuma zisizo sahihi. Inawajibika kuacha jambo hili na kutolijali. Bali amuombe Allaah ampe uzima mtoto wake kutokana na hayo wanayodai na ataona kheri kwa idhini ya Allaah.
Madaktari wengi hutamka mambo haya wakati bado ni kipanda cha damu au kinofu cha nyama. Yote hayo ni papara na madai ya batili. Muda wa mimba ni mrefu. Allaah humgeuza mtoto kutoka hatua moja kwenda nyingine na hali hubadilika. Kwa hivyo haijuzu kukimbilia katika jambo hilo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30978/ما-حكم-اسقاط-جنين-به-عاهة-في-الشهر-السابع
- Imechapishwa: 19/09/2025
Swali: Mwanamke anaumwa kisukari na shinikizo la damu na ni mjamzito wa miezi saba. Madaktari wamemwambia kwamba mtoto wake hana fuvu na atakufa mara tu atakapozaliwa. Je, inajuzu kuavya?
Jibu: Mambo haya hayatakikani kuyachukulia wepesi. Madaktari wengi husema mambo yasiyo ya kweli; inahusiana na dhuluma na tuhuma zisizo sahihi. Inawajibika kuacha jambo hili na kutolijali. Bali amuombe Allaah ampe uzima mtoto wake kutokana na hayo wanayodai na ataona kheri kwa idhini ya Allaah.
Madaktari wengi hutamka mambo haya wakati bado ni kipanda cha damu au kinofu cha nyama. Yote hayo ni papara na madai ya batili. Muda wa mimba ni mrefu. Allaah humgeuza mtoto kutoka hatua moja kwenda nyingine na hali hubadilika. Kwa hivyo haijuzu kukimbilia katika jambo hilo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30978/ما-حكم-اسقاط-جنين-به-عاهة-في-الشهر-السابع
Imechapishwa: 19/09/2025
https://firqatunnajia.com/kuavya-mimba-ya-miezi-saba-baada-ya-ushauri-wa-madaktari/