Kuacha kueneza elimu kwa kuchelea kujionyesha

Swali: Ambaye amepewa elimu na anachelea juu ya nafsi yake kujionyesha, je, inajuzu kwake kuacha kueneza elimu?

Jibu: Hapana, bali anapaswa kupambana na nafsi yake na kueneza elimu. Abul-´Abbaas Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ametaja kwamba hili ni miongoni mwa upotoshaji wa shaytwaan na kwamba humchanganya baadhi ya watu kwa kuacha kufanya matendo kwa kuogopa kujionyesha. Kwa hiyo baadhi ya wanazuoni wamesema kwamba kufanya jambo kwa ajili ya watu ni kujionyesha, na kuacha jambo kwa ajili ya watu ni kujionyesha na kwamba aliyehifadhiwa ni yule ambaye Allaah amemhifadhi kutokana na hayo mawili. Kwa hiyo muislamu apambane na nafsi yake kwa kufanya matendo. Ingelikuwa kila mmoja angeogopa kujioyesha na akaacha kufanya matendo, basi hakuna ambaye angefanya matendo.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
  • Imechapishwa: 07/10/2026