Swali: Ni ipi hukumu ya kunywa kinywaji cha shayiri ikiwa kina asilimiando ndogo kama mbili kwa mia ya alcohol?
Jibu: Mimi sijui kitu kuhusu kinywaji hicho. Lakini ikiwa kina asilimia kubwa ya alcohol ni haramu. Ama ikiwa kuna kitu kidogo ambacho hakionekani hakizingatiwi. Lakini hata hivyo ni jambo linahitajia kuangaliwa vizuri. Mtu huwezi kuhukumu kitu kabla ya kukiona. Mimi sijui kitu juu ya kinywaji hicho cha shayiri. Ikiwa hakina nyenzo zenye kulewesha hakina neno. Ama ikiwa kinywaji hicho kinapotengenezwa kinakuwa kingi na ndani yake kuna kitu kidogo, inaweza kusamehewa.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
- Imechapishwa: 01/03/2018
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Wafanyikazi wanampa msimamizi kinywaji
Swali: Mimi nafanya kazi kama msimamizi wa kikundi cha wafanyikazi. Inatokea wakati mwingine wananipa vinywaji. Je, inafaa kwangu kuvipokea? Jibu: Ikiwa wewe ndiye msimamizi na bosi wao, usikubali chochote kutoka kwao. Ni hongo. Wanakupa ili uwachukulie wepesi, uwasaidie na mfano wa hayo. Lakini ikiwa si wewe ndiye msimamizi wao, haina…
In "Rushwa - Hongo"
Kumzamisha nzi anapoingia kwenye kinywaji cha moto
Swali: Vipi ikiwa kinywaji ni cha moto? Jibu: Hata kama ni cha moto, udhahiri ni kuenea kwa hukumu. Hata hivyo mara nyingi ni kwamba nzi akiingia kwenye kinywaji cha moto mtu hawezi kufanya chochote. Mara nyingi ni kwamba hahitaji kukizamisha, kwa sababu kinateketezwa na moto. Mara nyingi huwa hivi. Mara…
In "Matibabu"
Tonge la mwisho la kusindikiza adhaana
Swali: Ni lini inalazimu kujizuilia na chakula? Je, ni kabla ya adhaana ya Fajr au baada yake? Je, mtu anapata dhambi ikiwa anajizuila wakati anaposikia adhaana? Jibu: Ikiwa anaona kuingia kwa alfajiri basi analazimika kujizuilia. Pindi kunapopambazuka alfajrii basi ni kama ambaye yuko jangwani anatakiwa kujizuilia pale anapoadhini muadhini. Kwa…
In "Daku"