Hamu kubwa ya watu hii leo kunywa pombe kunathibitisha utume wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kunamzidishie muislamu imani yake kumwamini Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Hebu nikuelezeni niliyosikia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambayo hakuna yeyote aliyasikia kutoka kwake ambaye atakusimulieni nayo baada yangu? Miongoni mwa alama za Saa ni kunyanyuliwa elimu, kuenea kwa ujinga na kudhihiri kwa uzinzi.”[1]

[1] Muslim (2671).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 259
  • Imechapishwa: 08/04/2025