Swali: Je, yale anayowahi mswaliji aliyekuja kuchelewa yanazingatiwa ndio ya sehemu yake ya mwanzo au sehemu yake ya mwisho?
Jibu: Maoni sahihi ni kwamba yale aliyowahi katika swalah yanazingatiwa ndio sehemu yake ya mwanzo na yale anayokidhi ndio sehemu yake ya mwisho. Kwa mfano akiwahi Rak´ah mbili za Dhuhr na akaweza kusoma Suurah nyingine baada ya al-Faatihah, atafanya hivo. Imamu anapotoa salamu, basi atasimama na kuswali Rak´ah zingine mbili na kusoma al-Faatihah peke yake. Kwa sababu yale anayokidhi ndio sehemu ya mwisho ya swalah yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kile mlichowahi kiswalini, na kile kilichokupiteni kikamilisheni.”[1]
[1] al-Bukhaariy (636) na Muslim (602).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/447)
- Imechapishwa: 12/04/2026
Swali: Je, yale anayowahi mswaliji aliyekuja kuchelewa yanazingatiwa ndio ya sehemu yake ya mwanzo au sehemu yake ya mwisho?
Jibu: Maoni sahihi ni kwamba yale aliyowahi katika swalah yanazingatiwa ndio sehemu yake ya mwanzo na yale anayokidhi ndio sehemu yake ya mwisho. Kwa mfano akiwahi Rak´ah mbili za Dhuhr na akaweza kusoma Suurah nyingine baada ya al-Faatihah, atafanya hivo. Imamu anapotoa salamu, basi atasimama na kuswali Rak´ah zingine mbili na kusoma al-Faatihah peke yake. Kwa sababu yale anayokidhi ndio sehemu ya mwisho ya swalah yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kile mlichowahi kiswalini, na kile kilichokupiteni kikamilisheni.”[1]
[1] al-Bukhaariy (636) na Muslim (602).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/447)
Imechapishwa: 12/04/2026
https://firqatunnajia.com/kile-alichowahi-mswaliji-aliyekuja-kuchelewa-ndio-sehemu-yake-ya-mwanzo-au-ya-mwisho/