Swali: Watu wanajua kuwa shirki ni haramu. Hata hivyo hawajui kuwa yale wanayoyafanya ndio shirki kutokana na ujinga wao…
Jibu: Shirki iko wazi na si kwamba haitambuliki. Shirki ni kumwomba asiyekuwa Allaah; kuchinja, kuweka nadhiri, kumwomba asiyekuwa Allaah na kuwataka msaada wafu. Hii ndio shirki. Kila mmoja anayajua haya.
Swali: Wengine ni watu wa kawaida na watu wazima…
Jibu: Watu wa kawaida na wazee wamesikia kuwa hayo wayafanyayo ni shirki kupitia kwa walinganizi, vitabu na redio. Wameyasikia haya, lakini hawataki kuachana nayo. Watu hawa hoja imeshawasimamia. Hoja ni ipi? Je, unataka kuingiza imani ndani ya mioyo yao? Hapana. Hoja ni kwa wewe kuwafikishia. Hoja imeshawafikia. Hata hivyo hawataki. Nini unachotaka kuwafanya?
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ad-Durr an-Nadhwiyd (01)
- Imechapishwa: 06/03/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket