Kikao kinachopendeza ndani ya swalah

Swali: Ni ipi hukumu ya wale wanaokaa kati ya Rak´ah ya kwanza na ya pili hata kama wako nyuma ya imamu?

Jibu: Kikao hiki huitwa kikao cha mapumziko (جلسة الاستراحة). Akiikaa kidogo baada ya Rak´ah ya kwanza na baada ya ya tatu basi hakuna neno. Kikao hiki kinapendeza kwa mujibu wa maoni yenye nguvu zaidi. Akikifanya hakuna ubaya, akifanya imamu, maamuma au anayeswali peke yake hakuna ubaya. Mwenye kukiacha pia hana dhambi. Imethibiti kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anakaa kikao chepesi baada ya Rak´ah ya kwanza na ya tatu kisha anasimama.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/296)
  • Imechapishwa: 07/03/2026