Kichwa kizima kinatakiwa kupunguzwa

Swali: Ukataji nywele unaofanywa baada ya ´Umrah ni kuchukua sehemu ya nywele kutoka kwenye kichwa kizima?

Jibu: Akate nywele sehemu yote ya kichwa; na sio kukata sehemu tu ya nywele. Akate nywele kichwa kizima kama anavyonyoa kichwa kizima. Allaah amefanya kupunguza badala ya kunyoa; kama ambavo kunyoa inakuwa kichwa kizima vivyo hivyo kupunguza. Leo mambo ni mepesi kuna mashine. Inawekwa kipimo fulani na inapunguza au kunyoa nywele zote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 03/07/2024