Kichinjwa kilichochinjwa makaburini

Swali: Katika nchi yetu wapo ambao wanachinja kwenye makaburi na wakati huohuo kunafanywa baadhi ya mambo ya shirki. Hilo likapelekea baadhi ya watu wakasema kuwa hawali kutoka kwenye vichinjwa vya nchi hio kwa sababu kuna uwezekano kichinjwa hicho kimechinjwa na wale wenye kufanya mambo hayo ya shirki. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Chenye kuchinjwa kwenye makaburi hakiliwi, kwa sababu kimechinjwa kujengea nia batili na mbovu. Ni kwa nini wanachinja kwenye makaburi? Si jengine ni kwa sababu wanayatukuza makaburi. Haijuzu kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/18073
  • Imechapishwa: 13/07/2019