Swali: Je, kuna katazo lolote imamu kumtanguliza mtu mwingine kuwaswalisha watu?

Jibu: Nilisema mara nyingi tulikuwa tukiona huko mji mkuu wa Syria, Dameski, tukimwona mtu anayeweza kuwa Khatwiyb mzuri, mwenye uwezo wa kuvutia nyoyo za wasikilizaji wake, hata hivyo hakuwa na ustadi wa kusoma vizuri. Kwa hivyo nilikuwa naona ni vyema kwamba mtu huyu awe Khatwiyb na ateue ambaye ana ustadi wa kusoma vizuri. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Awaongoze watu yule ambaye ni msomi zaidi wa Kitabu cha Allaah.”

Lakini, ikiwa Khatwiyb huyu amekusanya kati ya ufaswaha wa Khutbah yake na ustadi wa kusoma vizuri Qur-aan, basi haifai kumtanguliza mtu mwingine. Hii ni kwa sababu katika hali kama hii, mara nyingi, kitendo hicho huwa ni kwa ajili ya kujionyesha na hakufanywi kwa ajili ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).  Hata hivyo, ikiwa hatua ya kumtanguliza mwingine inafanywa kwa nia ya kufanikisha manufaa mawili – kwanza ni Khatwiyb mwenye uwezo mkubwa wa kuzungumza na pengine mtu huyo mwingine kuwaswalisha ndiye anayestahiki zaidi kutokana na ujuzi wake – basi katika hali hiyo itafaa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´abr-al-Haatif was-Sayyaarah (2)
  • Imechapishwa: 10/12/2024