Swali: Nini maana ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… asijipenyeze kati ya watu wawili… “[1]?

Jibu: Maana yake ni kwamba apange safu pale ilipoishilia safu. Asiwaudhi watu.

[1] Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ikiwa siku ya ijumaa ambapo mtu akaoga na akaosha kichwa chake, akajipata katika manukato yake mazuri na akavaa katika mavazi yake mazuri, kisha akatoka kwenda katika swalah, asijipenyeze kati ya watu wawili halafu akamsikiliza imamu, anasamehewa kutokea ijumaa hiyo mpaka ijumaa nyingine na ukiongezea siku tatu.” (Ameipokea Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23807/معنى-ولا-يفرق-بين-اثنين-في-الجمعة
  • Imechapishwa: 04/05/2024