Swali: Muulizaji anauliza kuhusu uhalali wa kula mnyama aliyekufa katika jangwa tupu, huku chakula kikiwa kimekatika kwa muda mrefu, lakini anayo maji ya kutosha ya kumfikisha katika maeneo yenye watu?

Jibu: Ikiwa amelazimika na akaogopa juu ya nafsi yake kufa asipokula, basi inajuzu kwake kula. Amesema (Subhaanah):

حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ وَأَن تَسْتَقْسِمُوا بِالْأَزْلَامِ ۚ ذَٰلِكُمْ فِسْقٌ ۗ الْيَوْمَ يَئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن دِينِكُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِ ۚ الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ فَمَنِ اضْطُرَّ فِي مَخْمَصَةٍ غَيْرَ مُتَجَانِفٍ لِّإِثْمٍ ۙ فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

”Mmeharamishiwa nyamafu na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa asiye Allaah katika kuchinjwa kwake na mnyama aliyekufa kwa kukosa hewa au aliyepigwa akafa au aliyeporomoka kutoka juu au aliyepigwa pembe na aliyeliwa na mnyama mwitu – isipokuwa mliyewahi kumchinja – na waliochinjwa kwa ajili ya ´ibaadah ya waabudiwa na kupiga ramli kwa mishale. Hayo kwenu ni ufuska. Leo wamekata tamaa wale waliokufuru na dini yenu, hivyo basi msiwaogope Niogopeni Mimi. Leo Nimekukamilishieni dini yenu na Nimekutimizieni neema Yangu na Nimekuridhieni Uislamu uwe dini yenu. Atakayedharurika katika njaa kali bila kulalia kwenye dhambi, basi hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

[1] 05:03

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (23/37)
  • Imechapishwa: 22/02/2026