Katika hali hii ndio itafaa kutumia Hadiyth dhaifu kwa mujibu wa Ibn Baaz

Swali: Ikiwa Hadiyth kwa mkusanyiko wa njia zake haipati nguvu ya kuwa nzuri kupitia nyengine na bado ikawa ni dhaifu – je, haitumiwi katika masuala ya kuzilainisha nyoyo?

Jibu: Hapana, haijathibiti kwa Sunnah, lakini inatumika kwa ajili ya kuhimiza tu – kwa mlango wa kuhimiza juu ya jambo lililothibiti. Ninachokusudia kwamba mfano ikiwa ni kuhusu swalah au wwawm, basi inahimizwa juu ya jambo lililothibiti.

Swali: Je, inajuzu kuifanyia kazi?

Jibu: Inakuwa kwa namna ya kuhimiza jambo, kwa njia ya kuhamasisha juu ya jambo lililothibiti. Yenyewe kama yenyewe haisimamishi hukumu yoyote. Hadiyth dhaifu haisimamishi hukumu yoyote, lakini inahimizwa kwayo juu ya hukumu zilizothibiti. Mfano wa mambo hayo ni fadhilah ya kufunga Ramadhaan, fadhilah ya kufunga siku ya ‘Arafah na fadhilah ya kufunga jumatatu na alkhamisi. Mambo haya yamethibiti kwa dalili sahihi. Hata hivyo mtu anaweza kutaja juu yake Hadiyth zinazokokoteza mambo hayo, kwa namna ya kuhimiza jambo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28483/ما-حكم-رواية-الحديث-الضعيف-والعمل-به
  • Imechapishwa: 20/04/2025