Katika hali hii leta Takbiyr-ul-Ihraam kisha sujudu

Swali: Mtu afanye nini akimkuta imamu amesujudu. Je, alete Takbiyr mbili au inatosha kuleta Takbiyrat-ul-Ihraam?

Jibu: Alete Takbiyrat-ul-Ihraam kisha ainame kwenda sujudu. Akileta Takbiyr mbili ni sawa. Muhimu ni kwamba Takbiyrat-ul-Ihraam inaletwa hali ya kuwa mtu amesimama.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 26/07/2019