Katika hali hii inafaa kwa mwanaume kuvaa hariri

625 – Nilimuuliza kuhusu kuvaa hariri wakati wa vita na Jihaad?

Jibu: Akanyamaza kidogo, kisha akasema kwamba inajuzu kwa sababu ya upele na kwa dharurah ikiwa hakupata nguo nyingine[1].

[1] Kufaa kwake kumepokewa na Shaykh-ul-Islam (28/27), (19/60) na akasema:

“Imepokelewa kutoka kwa ´Umar kwamba aliwatolea fatwa Maswahabah kuruhusu kuivaa wakati maadui walipoivaa.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 222
  • Imechapishwa: 14/06/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´