Karantini kwa mujibu wa Uislamu

Haijuzu kutoka nje ya nchi ambayo kumeenea majanga. Wala haijuzu kwa mtu kuingia ndani yake. Hivo ndivo ilivyo katika Hadiyth. Ikiwa kuna janga linaloenea katika nchi, basi usisafiri ndani yake. Rejea. Wakati tauni ilipotokea Shaam, basi ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alirejea kutoka Shaam. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtaposikia kuhusu tauni katika mji, basi msiingie ndani yake. Na ikitokea katika mji mliyomo, basi msitoke ndani yake kwa kuigopa.”[1]

Wale waliyomo ndani yake wanatakiwa kubakia humo. Wabakie humo na wala haifai kwa wao kutoka nje. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza jambo hilo. Pengine hekima ni maradhi yasienee. Jambo hilo huitwa karantini. Ni jambo ambalo liko na msingi.

[1] al-Bukhaariy (5729) na Muslim (2218).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://twitter.com/dralfawzann/status/1239135214124793858
  • Imechapishwa: 20/03/2020