Swali: Ni kipi kiumbe cha kwanza: kalamu au ´Arshi?
Jibu: Kiumbe cha kwanza kinachoonekana ni kalamu. Kuhusu viumbe kwa ujumla Allaah ndiye mjuzi zaidi. Wako wanazuoni waliosema kuwa ni ´Arshi. Maoni sahihi ni kwamba haitambuliki. Ibn-ul-Qayyim (Rahimhu Allaah) amesema:
Watu wametofautiana juu ya kalamu ambayo
makadirio yameitangulia kutoka kwa Hakimu
Je, ilikuwa kabla au baada ya ´Arshi?
kuna maono mawili kutoka kwa Abu ´Alaa´ al-Hamdaaniy
Sahihi ni kwamba ´Arshi ndio ilikuwa kabla
kwa sababu wakati wa uandishi ilikuwa na nguzo[1]
´Arshi ndio imeitangulia kalamu. Hata hivyo kalamu ndio kiumbe cha kwanza katika vinavyoonekana kama vile mbingu, ardhi n.k. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah ameandika makadirio ya viumbe miaka 50.000 kabla ya kuumba mbingu na ardhi na ´Arshi Yake ilikuwa juu ya maji.”[2]
[1] an-Nuuniyyah.
[2] Muslim (2653).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah (01)
- Imechapishwa: 13/05/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)