Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali ndani ya msikiti ambao kuna kaburi upande wa Qiblah?

Jibu: Haijuzu kuweka kaburi msikitini, si upande wa Qiblah chake, nyuma ya waswaliji, kuliani mwao wala kushotoni mwao. Ikiwa mtu amezikwa ndani ya msikiti, hata kama yeye ndiye mwanzilishi wa msikiti huo, kaburi hilo linatakiwa kufukuliwa na kuzikwa na pamoja na wengine. Ikiwa kaburi ndilo lililotangulia kuwepo kabla ya msikiti ambapo msikiti baadaye ukajengwa juu ya kaburi, basi ni lazima kuubomoa msikiti na utenganishwe mbali na kaburi. Mtihani wa makaburi kwenye misikiti ni kubwa sana. Pengine kaburi hilo likaanza kuabudiwa hata kama ni baada ya kupita muda mrefu. Huenda vilevile watu wakachupa mipaka juu yao au kutafuta baraka kutoka kwao. Jambo hili ni la khatari sana kwa waislamu. Lakini kaburi ndilo lililoanza kuwepo kabla ya msikiti basi ni lazima kuubomoa msikiti na kubadilisha maeneo yake. Ikiwa msikiti ndio ulioanza kujengwa kabla ya kaburi ni lazima kulifukua kaburi hilo na maiti huyo azikwe pamoja na waislamu wengine. Ni haramu na haisihi pia kuswali kwa kuliekea kaburi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiketi juu ya makaburi na wala msiswali kwa kuyaelekea.”[1]

[1] Muslim (972).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/374-375)
  • Imechapishwa: 03/03/2026