Swali: Ni lipi jukumu la waislamu kwa makundi potofu yaliyoenea miongoni mwao katika nchi zote ambayo lengo lao ni kuharibu ´Aqiydah ya muislamu? Na ni ipi nafasi ya wanazuoni kwao?

Jibu: Ni juu ya wanazuoni na watawala kuwapa nasaha, kuwaelekeza, kuwaamrisha mema na kuwazuia mabaya na kuzuia kuonekana kwa yale aliyoyaharamisha Allaah katika ´Aqiydah zao potofu. Wawape nafasi ya kutubia; asiyetubu anaweza kuadhibiwa hata kwa kupigwa au kufungwa gerezani ikiwa maslahi yanahitaji hivyo ili asiwadhuru watu kwa Bid´ah yake. Vivyo hivyo anayedhihirisha ufasiki na maasi; anazuiwa kwa nguvu ya dola kwa kupigwa au kufungwa ikiwa si katika mambo yenye kustahiki kutekelezewa adhabu ya kidini. Ama mambo yenye kustahiki kutekelezewa adhabu ya kidini hutekelezwa. Lakini anayefanya maasi kama kuwatukana watu au kuwasengenya, huyu anazuiwa kwa kile anachoona mtawala kinafaa, kama mfano wa kupigwa, kufungwa au vinginevyo. Watu wa ´Aqiydah potofu kama Raafidhwah, Mu´tazilah, Khawaarij na Suufiyyah wapotofu, wanashughulikiwa na mtawala kupitia wanazuoni kwa njia itakayozuia shari yao na kuikomesha; ama kwa kufungwa, kupigwa au kwa nasaha ikiwa itatosha na wakaacha shari yao na wakaonyesha kheri. Kwa kumalizia ni kwamba mambo yanapaswa kushughulikiwa kwa njia itakayozuia shari yake: iwe ni kufungwa, kupigwa, kufukuzwa nchini au kuuawa ikiwa Shari´ah inahitaji kuuawa kwake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3337/دور-المسلمين-نحو-الفرق-الضالة
  • Imechapishwa: 30/09/2026