Inatakiwa kutilia umuhimu elimu yenye manufaa kutokana na ile ´Aqiydah iliyomo ndani yake na kusoma “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na ya Muslim na vitabu vyengine vya Hadiyth. Maigizo haya ambayo yamewaharibu vijana yanatakiwa kukataliwa, kwa sababu dogo liwezelo kusemwa ni kwamba ni uwongo. Pengine mtu akawa pamoja na al-Ikhwaan al-Muslimuun au Jamaa´at-ut-Tabliygh kwa kipindi cha miaka arobaini ambapo baadaye akafa na huku yuko juu ya ´Aqiydah yake ya kizushi au ´Aqiydah yake ya kishirikina. Kwa hivyo ni jambo muhimu kuipatiliza ´Aqiydah. Ahl-us-Sunnah wanaitilia umuhimu ´Aqiydah na kuanza nayo. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomtuma Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anh) kwenda Yemen alimwambia:

“Hakika wewe unawaendea watu katika watu wa Kitabu. Hivyo basi iwe kitu cha kwanza utakachowalingania kwacho iwe ni kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah (na katika upokezi mwingine kwamba wampwekeshe Allaah pekee).”[1]

Ukimuuliza mmoja katika wakuu wao katika mabwana hawa ambaye haijui ´Aqiydah sahihi ni kwa nini anayapapasa makaburi, anajibu: “Tatizo liko wapi? Kwa sababu ni lazima kutoa kipaumbele kuwafanya waislamu kuwa na umoja.”

[1] al-Bukhaariy (1395) na Muslim (19).

  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 109
  • Imechapishwa: 12/02/2025