Josho la kawaida linamtosheleza kutohitajia kutawadha?

Swali: Nilioga josho la kawaida kisha nikaenda kuswali swalah ya ijumaa. Ni ipi hukumu ya hilo kwa kuzingatia pia kwamba sikutawadha?

Jibu: Swalah haisihi. Ni lazima kwako kutawadha na kurudi kuswali tena. Isipokuwa ikiwa ni josho la ijumaa au josho la janaba na wakati huohuo ukanuia kuondosha hadathi mbili baada ya kujisafisha kwa maji na hukutokwa na upepo wala hukugusa tupu yako kwa mkono. Josho hili linakutosheleza kutokana na maoni ya baadhi ya wanachuoni. Kuna maoni mengine yanayosema kuwa ni lazima kuoga.

Ama usiponuia au ilikuwa ni josho la kawaida tu – si josho la ijumaa wala josho la janaba – halikutoshelezi. Hivyo ni lazima kwako kurudi kutawadha na kuswali tena.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191589#219913
  • Imechapishwa: 21/03/2020