Josho la ijumaa linamtosheleza mtu kutokamana na kutawadha?

Swali: Je, josho la ijumaa linamtosheleza mtu kutokamana na kutawadha?

Jibu: Kuna tofauti. Baadhi ya wanachuoni wamesema kwamba mtu akinuia kuondosha hadathi mbili basi hadathi ndogo inaingia ndani ya hadathi kubwa. Wengine wakasema kuwa ni lazima kwa mtu kutawadha. Kwa hivyo lililo salama zaidi mtu aoge josho kamilifu, kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa akijisafisha, kisha akitawadha kwa ajili ya swalah, kisha akiosha kichwa chake, kisha upande wake wa kulia kisha upande wake wa kushoto. Hili ndio bora zaidi. Akigusa tupu yake au akatokwa na upepo arudi kutawadha tena. Hili ndio salama zaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/108/%D9%87%D9%84-%D9%8A%D9%83%D9%81%D9%8A-%D8%BA%D8%B3%D9%84-%D8%A7%D9%84%D8%AC%D9%85%D8%B9%D8%A9-%D8%B9%D9%86-%D8%A7%D9%84%D9%88%D8%B6%D9%88%D8%A1
  • Imechapishwa: 15/11/2019