Swali: Je, inafaa kufuata kipofu katika mambo ya ´Aqiydah?

Jibu: Hapana. Kufata kichwa mchunga inakuwa katika mambo ya Fiqh kwa ambaye ni mjinga. Amesema (Ta´ala):

فَاسْأَلُواْ أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لاَ تَعْلَمُونَ

“Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.”[1]

´Aqiydah hakuna kufuata kipofu. Ni lazima mtu ajifunze ´Aqiydah yake kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah na mfumo wa Salaf. Kuna vitabu vilivyothibitishwa,  vidogo na vikubwa. Vipo vitabu vinavyobainisha ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Chukua kwa mfano “al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah” ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah). Ni ´Aqiydah ilioenea inapokuja kubainisha ´Aqiydah na misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Mfano wake ni “at-Twahaawiyyah” ya Imaam at-Twahaawiy na maelezo yake mnayosoma hivi sasa.

[1] 16:43

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (73)
  • Imechapishwa: 09/04/2025