Swali: Ni ipi hukumu ya makundi na mapote mbalimbali ambayo ni yenye kutofautiana katika mifumo, ulinganizi na misingi yake, khaswa kwa kuzingatia kwamba kundi lililoshikamana na haki ni moja tu?

Jibu: Ni haramu na yamezuliwa. Muislamu anapaswa kujitenga nayo mbali na alinganie katika Qur-aan na Sunnah. Asifikiri mwenye kufikiri kuwa nahimiza mtu alinganie katika Uislamu peke yake – hapana, sifanyi hivo. Namuhimiza muislamu  ashirikiane na ndugu zake wote waislamu, waarabu na wasiokuwa waarabu, weupe na weusi. Kazi ya pamoja ni jambo linalotakikana. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

“… na wala msishirikiane katika dhambi na uadui.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mfano wa waumini, katika kupendana kwao, na kuhurumiana kwao na kuhisiana kwao, ni kama mfano wa mwili mmoja. Wakati kiungo cha mwili kinapatwa na maumivu, mwili mzima unapatwa na homa na kukosa usingizi.”[2]

Ikiwa Ahl-us-Sunnah watasimama kidete kulingania kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), basi vyamavyama vyote hivi vitaondoka, kwa sababu zimejengeka juu ya ubabaishaji na hadaa.

[1] 05:02

[2] al-Bukhaariy (6011) na Muslim (2586).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 391-392
  • Imechapishwa: 07/07/2025