Swali: Kuna aina fulani ya kitambara kinachoitwa ”jeans” na kinaweza kushonwa kwa aina tofauti juu ya mavazi ya watoto. Tatizo ni kwamba kitambara hichi huvaliwa na makafiri wanakifanya kuwa suruwali zenye kubana. Je, mtu akitumia kitambara hiki juu ya kitu kingine mbali na suruwali zenye kubana ina maana amejifananisha na makafiri?

Jibu: Kujifananisha maana yake ni mtu kufanya jambo ambalo ni maalum kwa yule anayejifananisha naye. Ikiwa kitambara hiki, au kitambara kingine, kitatumiwa kwa njia inayofanana na mavazi ya makafiri, basi kitendo hicho kimeingia katika kujifananisha. Hata hivyo hakuna neno mtu akatumia kitambara hicho kwa njia nyingine inayotofautiana na mavazi ya makafiri.

Swali: Ni ipi hukumu ya jeans juu ya mavazi ya watoto ikiwa itashonwa kwa njia niyngine?

Jibu: Ikiwa itashonwa kwa njia nyingine inayotofautiana na makafiri basi hakuna neno. Hakuna kujifananisha katika jambo la kitambara. Kwa sababu vitambara sio maalum vya kwao.

Swali: Hata kama wao ndio wameshuhurika kwavyo?

Jibu: Hata kama wao ndio wameshuhurika kwavyo muda wa kuwa sifa ya muonekano wake ni wenye kutofautiana na sifa ya muonekano wa makafiri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (16 B)
  • Imechapishwa: 13/12/2020