Swali: Je, inafaa kwa mwanaume kufunika bega lake moja wakati anaposwali?
Jibu: Ni jambo linalopendeza na sio lazima. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ikiwa ni yenye kubana, basi jifunge kiunoni mwako, na ikiwa ni pana, jizungushie nayo.”[1]
Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) aliswali na shuka yake ya chini na akaining´iniza juu shuka yake ya juu. Bwana mmoja akamuuliza juu ya hilo ambapo akasema:
“Nimefanya hivo ili aone mpumbavu kama wewe.”[2]
Imepokelewa katika tamko jengine:
“… ili waone wajinga.”
Haya ndio maoni yenye nguvu na ndio maoni ya jopo kubwa la wanazuoni.
Maoni yanayosema kuwa ni lazima aweke nguo katika moja ya bega lake haina maana kuwa bega ni uchi. Bali ni kwa sababu ya kukamilisha mavazi na kukaza kikoi. Hata hivyo bora zaidi ni kuswali ndani ya nguo mbili, kwa sababu ndio kunasitiri zaidi na salama zaidi. Imesihi kutoka kwa ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba amesema:
“Allaah akikukunjulieni, basi kunjukeni.”
Haya yanafahamisha kuwa mtu akiwa na wasaa, basi kuswali na nguo mbili ndio bora zaidi. Maneno yake ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) yanatiliwa nguvu na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa kama inafaa kwao kuswali ndani ya nguo moja, akasema:
“Je, hivi nyinyi nyote mna nguo mbili?”[3]
Haya yanafahamisha kuwa nguo moja inatosha, lakini Allaah akitufungulia basi tufunguke. Jengine ni kwamba maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Je, hivi nyinyi nyote mna nguo mbili?” yanafahamisha kuwa sio kila mtu ana nguo mbili. Bali watu wengi wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa na nguo moja tu.
[1] al-Bukhaariy na Muslim.
[2] Ahmad (3/335).
[3] al-Bukhaariy (358) na Muslim (515).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/293-294)
- Imechapishwa: 05/04/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/293-294)
Imechapishwa: 05/04/2026
https://firqatunnajia.com/je-ni-lazima-kwa-mwanamme-kufunika-bega-lake-moja-wakati-wa-kuswali/