Je, mwenye kukataa kutoa zakaah anakufuru japokuwa ataswali na kufunga?

Swali 46: Je, mwenye kukataa kutoa zakaah anakufuru japokuwa ataswali na kufunga?

Jibu: Hakufuru isipokuwa akiwa ni mwenye kupinga. Abu Bakr hakuwapiga vita baadhi yao kwa sababu wamekufuru. Lakini alisema iwapo watazuia kutoa kile walichokuwa wakikitoa kumpa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi nitawapiga vita kwacho.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 119
  • Imechapishwa: 24/09/2019