Je, maamuma wakae kikao cha kupumzika ikiwa imamu hakukaa?

Swali 25: Je, maamuma wakae kikao cha kupumzika[1] (جلسة الاستراحة) ikiwa imamu hakukaa?

Jibu: Maamuma anatakiwa kukaa kikao cha kupumzika ikiwa imamu hakukaa. Ni kama mfano wa kunyanyua mikono katika Takbiyrat-ul-Ihraam, baada ya kuinuka kutoka kwenye Rukuu´ au kuinuka kutoka katika Tashahhud ya kwanza japokuwa imamu yeye hatonyanyua.

[1] https://firqatunnajia.com/66-kikao-cha-kupumzika/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 36
  • Imechapishwa: 01/11/2018