Je, Adhkaar ni kwa mujibu wa dalili katika Qur-aan na Sunnah?

Swali: Je, Adhkaar ni kwa mujibu wa dalili katika Qur-aan na Sunnah?

Jibu: Nyiradi zinakuwa kwa njia ya kukomeka na kwa mujibu wa dalili za Kishari´ah. Kuna nyiradi ambazo zinakuwa kwa njia ya kukomeka ambazo kumepokelewa juu yake andiko. Mfano wake ni Tasbiyh, Tahliyl, Tahmiyd na Takbiyr. Kuna nyiradi zinazotokana na tafakuri na kutafakari, kama kumkhofu Allaah mtu anapokutana na jambo la kumtisha, kwa mfano kuwa na matumaini kwa Allaah, kuwa na shauku ya kukutana na Allaah, kukumbuka ukuu Wake na neema Zake kuu. Hizi mtu huzihitaji kulingana na tafakuri yake, akili yake, ukaribu wake na Allaah na kutokuwa na ughafilikaji. Kadhalika matendo mema ambayo Allaah ameyaweka katika Shari´ah ambayo mtu anatakiwa kujikurubisha kwayo kwa kuyafanya kama alivyoweka Allaah, kama swalah na mengineyo. Kwa hiyo ´ibaadah ni kwa mujibu wa dalili. Hata hivyo njia za kuzifikia zinatofautiana.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31186/هل-الاذكار-توقيفية-وما-انواع-الذكر
  • Imechapishwa: 10/10/2025