Je, adhabu ya ndani ya kaburi ni endelevu au yenye kukatika?

Swali: Je, adhabu ya ndani ya kaburi ni endelevu au yenye kukatika?

Jibu: Akiwa ni kafiri basi adhabu yake inakuwa yenye kuendelea na hakuna namna yoyote ile ya kuneemeshwa. Lakini akiwa ni mtenda madhambi muumini, basi akiadhibiwa ndani ya kaburi lake anaadhibiwa kwa kiwango cha madhambi yake. Huenda kuadhibiwa kutokana na madhambi yake kukawa kudogo kuliko kile kituo (البرزخ) ambacho kinakuwa kati ya kifo chake na kusimama kwa Qiyaamah. Kwa msemo mwingine inakuwa ni adhabu yenye kukatika.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mjamuu´-ul-Fataawaa (17/436-437)
  • Imechapishwa: 29/05/2026