Swali: Kuhusu mtu anayeswali kwa kulazimishwa anakufaa hali ya kuwa kafiri ikiwa atakufa katika hali hiyo?
Jibu: Makusudio ni kwamba ikiwa hakuswali kwa ajili ya Allaah, bali akaswali kwa ajili ya viumbe, basi swalah yake haikubaliwi.
Swali: Vipi kuhusu yule anayelazimishwa kuswali kwa nguvu?
Jibu: Allaah amesema:
فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا
“Hivyo anayetaraji kukutana na Mola wake na atende matendo mema na wala asishirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote!”[1]
Ni lazima kitendo kiwe kwa ajili ya Allaah pekee.
Swali: Je, kuna faida gani baba kumlazimisha mwanawe aswali?
Jibu: Hilo ni kusaidiana katika wema, kama Allaah anavyosema:
وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ
“Saidianeni katika wema na uchaji Allaah.”[2]
Ikiwa ataswali kwa ajili ya Allaah kwa sababu baba yake amemuamuru, huko sio kujionyesha. Bali ameswali kwa ajili ya Allaah kwa kufuata amri ya baba yake. Kama Allaah alivyosema:
وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ حَكِيمٌ
“Waumini wanaume na waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao: wanaamrisha mema na wanakataza maovu.”[3]
Mwanadamu anapaswa kupambana na kusaidiwa dhidi ya nafsi yake.
[1] 18:110
[2] 05:02
[3] 09:71
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31361/ما-حكم-من-يصلي-رغما-عنه-او-لامر-ابيه
- Imechapishwa: 22/10/2025
Swali: Kuhusu mtu anayeswali kwa kulazimishwa anakufaa hali ya kuwa kafiri ikiwa atakufa katika hali hiyo?
Jibu: Makusudio ni kwamba ikiwa hakuswali kwa ajili ya Allaah, bali akaswali kwa ajili ya viumbe, basi swalah yake haikubaliwi.
Swali: Vipi kuhusu yule anayelazimishwa kuswali kwa nguvu?
Jibu: Allaah amesema:
فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا
“Hivyo anayetaraji kukutana na Mola wake na atende matendo mema na wala asishirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote!”[1]
Ni lazima kitendo kiwe kwa ajili ya Allaah pekee.
Swali: Je, kuna faida gani baba kumlazimisha mwanawe aswali?
Jibu: Hilo ni kusaidiana katika wema, kama Allaah anavyosema:
وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ
“Saidianeni katika wema na uchaji Allaah.”[2]
Ikiwa ataswali kwa ajili ya Allaah kwa sababu baba yake amemuamuru, huko sio kujionyesha. Bali ameswali kwa ajili ya Allaah kwa kufuata amri ya baba yake. Kama Allaah alivyosema:
وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ حَكِيمٌ
“Waumini wanaume na waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao: wanaamrisha mema na wanakataza maovu.”[3]
Mwanadamu anapaswa kupambana na kusaidiwa dhidi ya nafsi yake.
[1] 18:110
[2] 05:02
[3] 09:71
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31361/ما-حكم-من-يصلي-رغما-عنه-او-لامر-ابيه
Imechapishwa: 22/10/2025
https://firqatunnajia.com/inakubaliwa-swalah-ya-anayeswali-baada-ya-kuamrishwa-na-mtu-mwengine/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket