Inajuzu kwa mfungaji kunusa harufu ya manukato na udi?

Swali: Inajuzu kwa mfungaji kunusa harufu ya manukato na udi?

Jibu: Asivute/nuse udi. Ama aina nyenginezo za manukato, mbali na vile vyenye moshi, hazina neno. Lakini udi wenyewe asivute harufu yake. Kuna baadhi ya wanachuoni ambao wanaona kuwa mfungaji akivuta/nusa harufu ya udi basi amefungua. Kwa sababu unaenda kwenye ubongo wake. Isitoshe una harufu kali. Ama akinusa pasi na kukusudia hakumfunguzi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/266)
  • Imechapishwa: 26/05/2018