Swali: Imethibiti kukatazwa wanawake kutembelea makaburi. Je, wanaruhusiwa kushiriki kwenye mazishi au hapana?

Jibu: Kumswalia maiti si tatizo. Wanawake wanaweza kumswalia maiti. Wanawake waliswali pia juu ya jeneza la Mtume (Swalla Allaahu ʿalayhi wa sallam). Lakini wanachokatazwa ni kumsindikiza maiti kwenda makaburini na kutembelea makaburi. Haya wamekatazwa. Hawafuati jeneza mpaka makaburini wala hawatembelei makaburi. Hicho ndicho kilichokatazwa. Lakini kuwaswalia maiti pamoja na watu, hilo ni jambo limesuniwa na ni jema.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1151/حكم-صلاة-النساء-على-الميت-وتشيعيهن-للجناىز
  • Imechapishwa: 03/01/2026