Swali: Mtu akiwa njiani afupishe swalah ya ijumaa au aiswali Rak´ah nne kwa sababu tumesikia kutoka kwako ya kwamba haijuzu kwa mtu kufupisha swalah ya ijumaa wala kuijumuisha pamoja na ´Aswr? Ni upi sahihi wa nukuu hii?
Jibu: Nukuu kwa sura kama hii ni uongo na mimi sijasema maneno haya.
Kuhusu kwamba ijumaa haifupishwi ni kweli. Ijumaa ikifupishwa itakuwa Rak´ah moja tu, jambo ambalo halikusemwa na mwanachuoni yeyote wala hakuna hata mjinga anayesema hivo. Ijumaa haifupishwi. Inaswaliwa vilevile Rak´ah mbili. Msafiri akipita katika mji siku ya ijumaa na akatua hapo na akasema kuwa ataendelea na safari yake jioni na swalah ya ijumaa ikamkuta hapo, haifai akaijumuisha pamoja na ´Aswr. Ijumaa ni swalah ya kipekee, ilio na masharti maalum na sifa maalum. Sunnah imekuja kujumuisha kati ya Dhuhr na ´Aswr ambapo ijumaa sio Dhuhr. Kwa ajili hii si sawa kujumuisha ijumaa na ´Aswr. Ambaye alijumuisha ijumaa na ´Aswr tunamwambia arudi kuswali ´Aswr Rak´ah mbili baada ya kuingia wakati wake.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (25)
- Imechapishwa: 18/01/2019
Swali: Mtu akiwa njiani afupishe swalah ya ijumaa au aiswali Rak´ah nne kwa sababu tumesikia kutoka kwako ya kwamba haijuzu kwa mtu kufupisha swalah ya ijumaa wala kuijumuisha pamoja na ´Aswr? Ni upi sahihi wa nukuu hii?
Jibu: Nukuu kwa sura kama hii ni uongo na mimi sijasema maneno haya.
Kuhusu kwamba ijumaa haifupishwi ni kweli. Ijumaa ikifupishwa itakuwa Rak´ah moja tu, jambo ambalo halikusemwa na mwanachuoni yeyote wala hakuna hata mjinga anayesema hivo. Ijumaa haifupishwi. Inaswaliwa vilevile Rak´ah mbili. Msafiri akipita katika mji siku ya ijumaa na akatua hapo na akasema kuwa ataendelea na safari yake jioni na swalah ya ijumaa ikamkuta hapo, haifai akaijumuisha pamoja na ´Aswr. Ijumaa ni swalah ya kipekee, ilio na masharti maalum na sifa maalum. Sunnah imekuja kujumuisha kati ya Dhuhr na ´Aswr ambapo ijumaa sio Dhuhr. Kwa ajili hii si sawa kujumuisha ijumaa na ´Aswr. Ambaye alijumuisha ijumaa na ´Aswr tunamwambia arudi kuswali ´Aswr Rak´ah mbili baada ya kuingia wakati wake.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (25)
Imechapishwa: 18/01/2019
https://firqatunnajia.com/inafaa-kwa-msafiri-kukusanya-kati-ya-ijumaa-na-aswr-ii/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket