Swali: Imethibiti kuwa katika majina ya Allaah ni Mzuri (al-Jamiyl)?

Jibu: Ndio. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika ya Allaah ni Mzuri (al-Jamiyl) na anapenda uzuri.”

Imepokelewa na al-Bukhaariy na Muslim

Swali: Mtu anaweza kujiita “´Abdul-Jamiyl”?

Jibu: Mzuri ni jina la Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala). Lakini hata hivyo ajiite kwa majina ambayo yako wazi yasiyokuwa na utata. Hili ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah (01)
  • Imechapishwa: 09/08/2020