Imamu kusoma Aayah hizi katika Khutbah ni Bid´ah?

Swali: Je, kusoma Aayah:

إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ

“Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Mtume… ”

na:

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ

“Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na wemaa na kuwapa [mahitajio na msaada] jamaa wa karibu… ”[1]

kila Khutbah ni Bid´ah? Kwa sababu maimamu huendelea kuzisoma Aayah hizi mara kwa mara?

Jibu: Sioni tatizo katika hilo. Kwa sababu Aayah ya kwanza ni himizo la kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwaita waislamu wamswalie Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuhusu Aayah ya pili ni Aayah yenye ujumbe mpana, inayokusanya kheri nyingi na ni mawaidha na ukumbusho kwa waislamu. Hivyo basi kusomwa kwake katika Khutbah ni katika mawaidha.

[1] 16:90

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1459/حكم-مداومة-الخطيب-على-ان-الله-وملاىكته-يصلون-على-النبي
  • Imechapishwa: 19/02/2026