Imamu hakusoma Suurah nyingine baada ya al-Faatihah

Swali: Ni ipi hukumu ya imamu ambaye amewaswalisha watu mkusanyiko katika swala ya kusoma kwa sauti na hakusoma kitu baada ya al-Faatihah?

Jibu: Swalah ni sahihi. Kilicho cha lazima ni kusoma al-Faatihah. Ni nguzo katika swalah. Chenye kuzidi juu ya al-Faatihah kimependekezwa. Lakini inatakiwa kwa mtu afanye kile kilichopendekezwa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 05/07/2020