Swali: Katika swalah ya Rak´ah nne imamu alisimama kwenda Rak´ah ya tano kwa kusahau ambapo baadhi ya wanaoswali wakamfuata na wengine wakabaki wamekaa mpaka akaswali Rak´ah ya tano kisha akasalimu. Ni yupi aliyefanya sahihi?
Jibu: Swalah yao yote ni sahihi. Yule aliyesimama kwa ujinga, swalah yake ni sahihi. Wale waliotambua kwamba ni Rak´ah ya ziada wakangoja mpaka imamu amalize, swalah yao pia ni sahihi – na huo ndio uliokuwa wajibu wao. Ikiwa maamuma anajua kwamba ni Rak´ah ya ziada basi hatakiwi kusimama. Bali anakaa na anangoja mpaka imamu asalimu. Anapaswa kumtanabahisha yule asiyejua ili asisimame kumfuata imamu. Kwa sababu msingi ni kumfuata imamu. Wote swalah zao ni sahihi – Allaah akitaka.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/165)
- Imechapishwa: 07/03/2026
Swali: Katika swalah ya Rak´ah nne imamu alisimama kwenda Rak´ah ya tano kwa kusahau ambapo baadhi ya wanaoswali wakamfuata na wengine wakabaki wamekaa mpaka akaswali Rak´ah ya tano kisha akasalimu. Ni yupi aliyefanya sahihi?
Jibu: Swalah yao yote ni sahihi. Yule aliyesimama kwa ujinga, swalah yake ni sahihi. Wale waliotambua kwamba ni Rak´ah ya ziada wakangoja mpaka imamu amalize, swalah yao pia ni sahihi – na huo ndio uliokuwa wajibu wao. Ikiwa maamuma anajua kwamba ni Rak´ah ya ziada basi hatakiwi kusimama. Bali anakaa na anangoja mpaka imamu asalimu. Anapaswa kumtanabahisha yule asiyejua ili asisimame kumfuata imamu. Kwa sababu msingi ni kumfuata imamu. Wote swalah zao ni sahihi – Allaah akitaka.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/165)
Imechapishwa: 07/03/2026
https://firqatunnajia.com/imamu-anayesimama-katika-rakah-ya-tano/