Swali: Je, inafaa kuswali swalah ya faradhi nyuma ya anayeswali swalah inayopendeza?
Jibu: Maoni sahihi ni kwamba haidhuru kule kutofautiana kwa nia ya imamu na maamuma. Vilevile inafaa kwa ambaye anaswali swalah ya faradhi kuswali nyuma ya anayeswali swalah ya inayopendeza. Mu´aadh bin Jabal alikuwa akiswali pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) swalah ya ´Ishaa ambapo anarejea kwa watu wake na kuwaswalisha swalah hiyohiyo[1]. Kwake inakuwa ni swalah ya kujitolea na kwa wao inakuwa ni swalah ya faradhi. Kwa hivyo akiingia mtu msikitini na wewe unaswali swalah ya faradhi au swalah ya kujitolea na akajiunga nawe ili mswali mkusanyiko, hapana vibaya. Swalah yenu ni sahihi. Mwache ajiunge nawe na aswali kile atachokidiriki kwako. Ukimaliza kuswali yeye atasimama na kukidhi kile kilichobakia kwake ikiwa kumebaki kitu, ni mamoja ulikuwa unaswali swalah ya kujitolea au swalah ya faradhi.
[1] al-Bukhaariy (701).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/452)
- Imechapishwa: 13/04/2026
Swali: Je, inafaa kuswali swalah ya faradhi nyuma ya anayeswali swalah inayopendeza?
Jibu: Maoni sahihi ni kwamba haidhuru kule kutofautiana kwa nia ya imamu na maamuma. Vilevile inafaa kwa ambaye anaswali swalah ya faradhi kuswali nyuma ya anayeswali swalah ya inayopendeza. Mu´aadh bin Jabal alikuwa akiswali pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) swalah ya ´Ishaa ambapo anarejea kwa watu wake na kuwaswalisha swalah hiyohiyo[1]. Kwake inakuwa ni swalah ya kujitolea na kwa wao inakuwa ni swalah ya faradhi. Kwa hivyo akiingia mtu msikitini na wewe unaswali swalah ya faradhi au swalah ya kujitolea na akajiunga nawe ili mswali mkusanyiko, hapana vibaya. Swalah yenu ni sahihi. Mwache ajiunge nawe na aswali kile atachokidiriki kwako. Ukimaliza kuswali yeye atasimama na kukidhi kile kilichobakia kwake ikiwa kumebaki kitu, ni mamoja ulikuwa unaswali swalah ya kujitolea au swalah ya faradhi.
[1] al-Bukhaariy (701).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/452)
Imechapishwa: 13/04/2026
https://firqatunnajia.com/imamu-amekusudia-swalah-maamuma-amekusudia-swalah-nyingine/