Swali: Vipi ikiwa nitaswali Rak´ah nne na imamu ambapo akasahau na kuinuka katika Rak´ah ya tano?

Jibu: Msubirie, usisimame naye. Msubirie hadi atakapoikaa na kutoa salamu pamoja naye. Sema:

سبحان الله سبحان الله

”Allaah ametakasika na mapungufu. Allaah ametakasika na mapungufu.”

Asipokusikiza, basi wewe na wale wanaojua kuwa amezidisha ketini chini. Msisimame pamoja naye. Akimaliza kuswali na akatoa salamu, basi nanyi mtatoa salamu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1222/هل-يجوز-متابعة-الامام-اذا-زاد-في-الصلاة
  • Imechapishwa: 07/02/2026